EXHIBITS
Mradi wa Usambara: Mandhari ya Mabadiliko na Endalevu katika Milima Usambara ya Mashariki, c. 1910: Mazingira ya Milima ya Usambara
English
Mazingira ya Milima ya Usambara
Historia ya Asili
Milima ya Usambara ni sehemu ya Milima ya Tao la Mashariki, ambayo inaanzia kusini mwa Kenya hadi kusini mwa Tanzania. Miinuko ni ya zamani, tukizungumza kijiolojia. Iliundwa takribani miaka milioni mia moja iliyopita ikitengeneza milima na mambonde kwenye mstari wa zamani wa mabonde. Milima hiyo inainuka juu ya tambarare zinazozunguka na kama safu za pwani na hupata mvua za monsuni zinazonyesha katika Bahari ya Hindi. Mvua thabiti za msimu, hata wakati wa kipindi cha mamilioni ya miaka ya miamba[Pleistocene], ilikuza ukuaji wa misitu ya Uwoto wa asili {tropical}katika Mikoa ya Mashariki. Mwinuko na viwango vya joto pia vilikuza anuwai ya viumbe hai{kibaolojia} kwa kipindi kifupi sana, hivyo kwamba taasisi ya kisayansi inachukulia misitu ya milima kuwa maeneo yenye anuwai ya kibaolojia ya ulimwengu na maadili ya juu ya uhifadhi.